ITAMBUE SONONA(DEPRESSION)
Sonona(Depression) ni mojawapo ya magonjwa ya akili ambayo madhara yake katika mustakabali wa maisha ya mtu binafsi pamoja na watu wanaomzunguka sio mazuri sana,madhara haya huweza kuleta hali ya sintofahamu kwa watu wanaomzunguka mtu aliye katika hali hiyo wakati mtu mwenyewe aliye katika hali ile hujiona kawaida kwa kuwa ndio hali inayomfanya ajisikie ahueni. Sonona(Depression ) ni hisia za huzuni na masononeko azipatazo mtu kutokana na matokeo ya mifumo mbalimbali ya maisha kama vile mahusiano,shule,kazi na mambo mengine yanayochukua nafasi ya muhimu katika maisha ya mtu binafsi. Hisia hizi ambazo mara nyingi huwa katika mfumo hasi,hutokana na matokeo yasiyotarajiwa na mtu katika jambo fulani ambalo anaweza kuwa alilipa nafasi kubwa sana katika maisha yake,lakini jambo hilo likatokea kuwa tofauti na kuingilia au kuvuruga kwa kiasi kikubwa mfumo wa kufikiria na kutenda wa mtu. Zitambue dalili za mtu mwenye Sonona(Depression) Kujisikia huzuni na maumivu ndani ya nafsi(Dep...