NINI CHANZO CHA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO?
Katika maisha ya kila siku ya viumbe hai,hali ya ukaribu huonekana zaidi mara kwa mara. Ukaribu huu huweza kusababishwa na mazingira waliyomo,vitu wanavyofanya na mambo wanayopenda kwa pamoja.Lakini kwa binadanu hali ya ukari husababishwa na malengo maalumu kati ya mtu na mtu,ukaribu huo huweza kusababishwa na vitu tofauti tofauti vinavyoendana kati ya mtu na mtu kama vile malengo,mitazamo,upendo,uhitaji,hisia na mambo mengine mengi yanayoweza kuwa sehemu kubwa ya kuwaleta watu karibu.
Mahusiano haya au ukaribu huu unaweza kuwa wa aina tofauti kutegemeana na dhamira iliypo kati ya watu wawili,na ndipo hapo tunapata mahusiano ya kifamilia,ya kimapenzi,ya kikazi,ya kijamii,ya kirafiki na aina nyingine zote kutegemeana na dhamira pamoja na malengo yenu.
Migogoro ni kitu ambacho huweza kwa kiasi kikubwa sana kudumisha ama kuzorotesha na hata kuharibu kabisa mahusiano kati ya mtu,na si watu au binadamu pekee lakini pia hata wanyama na viumbe wengine pia hukumbana na changamoto ambazo hupelekea kujikuta wakiwa katika migogoro.
Na migogoro hii ni kitu kisichoepukika kabisa katika mahusiano kutokana na baadhi sababu ya sababu nilizotaja hapo juu.Migogoroni katika mahusiano ni hali ya kutofautiana,kimawazo kimtazamo,kimsimamo,kimalengo,kihisia kati ya watu wawili walioko katika mahusiano.na kupitia tofauti hiyo kila mmoja hupigana ili kuweza kueleweka kwa jinsi anavyotaka yeye.Katika mahusiano migogoro ni kitu cha kawaida na ambacho hakiepukiki,lakini migogoro hii hutakiwa kuwa ya faida zaidi kuliko hasara zaidi.Migogoro katika mahusiano huwa mizuri au na faida kwa kuwa husaidia kaika haya yafuatayo kati ya mengine;
- Husaidia kutengeneza na kuimarisha uelewano wa hali ya juu kati ya watu wawili,kwani kupitia migogoro kila mtu anajitahidi kuelezea hisia yake juu ya chanzo kikuu.
- Huleta, hujenga na kuongeza heshima kati ya watu wawili walio katika mgogoro.
- Huleta,hutengeneza na kudumisha heshima kati ya watu walioko katika mgogoro.
Hivyo ili maisha yaendelee vizuri na mahusiano yaweze kudumu,migogoro hutakiwa kuchukuliwa kama sehemu ya maisha.Na huweza kuonekana ya faida zaidi hasa pale unapoyachukulia katika mtazamo chanya.
Vyanzo mbalimbali vya migogoro katika mahusiano
- Uhitaji: Kila binadamu katika maisha yake ya kila siku ana mahitaji yake anayohitaji ili maisha yaweze kuendelea,vivyo hivyo katika mahusiano baina ya watu wawili kila mtu an uhitaji wake.Uhitaji kati ya mtu na mtu hauwezi kuwa unafanana hata siku moja,unaweza kufanana kwa kuskia lakin ukatofautiana kwa uhalisia.Hivyo tofauti ya uhitaji kati ya watu walioko katika mahusiano huweza kusababisha migogoro kutokea.
- Mtazamo: Binadamu siku zote hatupo sawa kwa kila kitu,isipokua huendana kwa baadhi ya vitu tu.Kila mtu huwa na mtazamo tofauti juu ya kila kitu au kila jambo linalotokea katika maisha yetu ya kila siku,kitendo cha kuwa na imani hasa pale mnapokuwa katika mahusiano kuwa mnaendana kwa kila kitu huweza kuleta migogoro pale mnapokuta mnatofautina kimtazamo juu ya jambo au hali fulani iliyopo mbele yenu.
- Maoni: Maoni juu ya jambo au hali fulani ni kitu cha muhimu sana katika kudumisha na kuimarisha mahusiano,lakini maoni haya inapotokea yakawa tofauti na mwenzio au hayaendani na mwenzio anachokitazamia huweza kuleta kadhia katika mahusiano yenu. Maoni juu ya nini kifanyike yanaweza kuwa tofauti na jinsi gani kifanyike,hatima yake kushindwa kuelewana kati ya pande mbili.
- Imani:Imani ni nguzo kubwa na ya muhimu san katika kuimarisha mahusiano,na hii imani hii si lazima iwe inatokana ama na dini yako au unavyotakiwa kufanya kwa mujibu wa mila na desturi.Lakini hii imani hii huusisha jinsi gani unavyomchukulia mwenzako katika mahusiano yenu.Mwingine huweza kuaminikuwa ili mahusiano yao yadumu ni lazima kwenda kwa mganga wa jadi kila baada ya mwezi,lakini kwa upande wa mwenzaie ni tofauti kabisa.Hivyo hali hii ya kutofautiana huweza kuleta migogoro kwa asilimia kubwa sana.
- Thamani: Kila binadamu katika hii dunia ana kitu anachokipa nafasi kubwa asana katika maisha yake na kukifanya kuwa na thamani zaidi.Na vitu hivi hutofautiana kati ya mtu na mtu ambapo mwenzio anaweza ona hiki kina thamani kwake lakini wewe ukaona ni cha nini kwako.Hali hii huwa tofauti hasa pale watu wawili waliopo katika mahusiano wanapotambua kuwa mimi pesa ni za thamani sana kwangu na mwingine akatambua kuwa mapenzi ni ya thamani zaidi kwake kulko pesa.Mwisho wa yote hayo lazima kutatokea kutoelewana baina ya watu hao wawili.
- Vipaumbele: Katika maisha ya kila siku kila mtu ana kitu au vitu an hata mambo ambayo huyapa nafasi ya juu sana katika maisha yake,na hapo ndipo utakuta kuna watu hutoa nafasi ya juu sana katika starehe,wengine katika kujenga nyumbana hata wengine katika kula.Hii ni hali ya kawaida sana,lakinikatika mahusiano vipaumbele huwekwa baina ya watu wawili waliopo katika mahusiano,lakini vipaumbele hivi inapotokea kutofautiana kati yao wawili huweza kuleta kutokuelewana baina yao.
Hizo ni sababu za jumla bila kujalishaaina ya uhusiano ulio nao kati yako na mwenzio.Kuna sababu nyingine nyingi ndogo ndogo lakini ni za muhimu ambazo huweza kusababisha migogoro katika mahusiano kutegemeana na aina ya uhusiano.
Hatua muhimu katika kutatua migogoro ndani ya mahusiano
- Tambueni chanzo au hali sababishi ya mgogoro uliopo.Fanyeni majadiliano ya pamoja baina yenu kwa kuangalia mitazamo yote hasi na chanya baina ya pande zote mbili,hii itasaidia kila mtu kutambua hisia za mwenzake juu ya tatizo lilipo.
- Tengenezeni kwa pamoja njia mbadala za kulitatua tatizo lilipo.Hii hufanyika kwa kila mmoja kumpa mwenzie nafasi ya kutoa wazo alilonalo juu ya nini kifanyike ili kufikia muafaka wa tatizo lililopo baina yenu.Angalieni malengona makubaliano yenu juu ya mahusiano yenu,hii itasaidia katika kupata suluhisho mapema.
- Chambueni kwa umakini zaidi njia mbadala mlizo chagua ili ziwasaidie katika kupata muafaka wa mgogoro uliopo. Ondoeni njia mnazoona kuwa haziwezi kuleta muafaka wowote ule,hakikisheni mmepata njia mbili ama tatu zitakazo waongoza katika kupata muafaka wa nini kifanyike.
- Baada ya hapo amueni kwa pamoja na kwa moyo mmoja njia bora na sahihi zaidi kati ya zote,njia hiyo ikubalike kwa pamoja na ndio itumike katika kupata suluhisho la mgogoro mliopo nao.
- Mwisho ni kuhakikisha kila mmoja wenu anafanya ufuatiliaji kwa mwenzie kama njiailiyokubalika inatumika ipaswavyo,na wakatimwingine ni vizuri kuongelea kwa pamoja juu ya nini kinachoendelea.
Kumbuka: Katika mahusiano ni vizuri sana kuutazama mgogoro wowote ule kwa pamoja na kwa mtazamo chanya,na hapo ndipo mtaweza kujifunza jinsi gani ya kukabiliana na chanagmoto yoyote ile.Kuepuka ama kuogopa migogoro ni katika mahusiano ni sawa kuchagua kuogopa kuongelea mambo ya muhimu katika mahusiano yenu na mwisho wake itakuwa ngumu pia kutambua hisia zenu kwa pamja juu ya mambo tofauti mnayokutana nayo katika maisha ya kila siku.
Mambo ya kuepuka
- Epuka kuto-kujadili na mwenzio juu ya njia unazohisi zinafaa katika kutatua migogoro mnayokutana nayo katika mahusiano yenu.
- Kuchelewa kutambua mapema taarifa muhimuzinazopelekea mgogoro kutokea baina yenu.
- Kujipendelea na kujiangalia kwa kiasi kikubwa peke yako kwa kufanya kile kisicholeta usawa baina yako na mwenzio.
- Kusahau kuwa kuna njia nyingi na tofauti za kufanya vitu,na si kuamini tu kila unachokiona kinafaa ndicho cha sahihi kwa wakati huo.
- Kuangalia zaidi juu ya nini unachopoteza wewe binafsi na si nini mtachopata wewe na mwenzio.
- Kuamini zaidi kuwa ni lazima mwenzio apote ili wewe ufanikiwe.
- Kuingiza mambo mengine katika mambo ya msingi mliyokubaliana na mwenzio kuyakamilisha kwa wakati fulani.
Kumbuka: Mgogoro siku zote huwa mkubwa zaidi katika mahusiano hasa pale makubaliano yasipofikiwa kati ya mtu na mtu,na mwitikio wa mgogoro katika mahusiano hutokana zaidi na mtazamo unaokuwepo juu ya tatizo.
MWISHO!!!!!!
Kwa lolote na chochote usisite kunitafuta kwa njia yoyote ya mawasiliano kama ilivyoandikwa hapo juu
Comments
Post a Comment