NI NINI CHANZO CHA HASIRA

Acid ni kemikali ambayo ni hatari sana,kemikali hii inapowekuwa katika chombo huathir zaidi chombo hicho kuliko vitu vingine vyote vilivyopo jirani na chombo hicho.
Vivyo hivyo ndivyo mtu anapokuwa na hasira,kwani hasira ni hali ambayo humuathiri zaidi aliyenayo kuliko mtu mwingine zaidi,kwani maumivu ya hasira huyapata yle aliyenayo zaidi kuliko aliyechanzo cha hasira hiyo.
Kila kiumbe aliye hai hupatwa na hasira,yaani wanyama,ndege na hata wadudu wote hupatwa na hasira.Hivyo hasira ni hali isiyoepukika katika hali ya kawaida.
Mwanasaikolojia T.W Smith  yeye alisema kuwa,hasira ni muhemko usio epukika,muhemko huu unaotokana na hisia hasi juu kitu,jambo au hali fulani.Nuhemkohuu hutofatiana kutoka katika hali ya kawaida hadi katika hali inaweza kusababisha madhara kwa mtu binafsi na hata kwa watu wengine.
Image result for Anger

Binadamu ndiye kiumbe amabaye hupatwa na hasira mara kwa mara kuiko viumbe wengine wote,na hasira hii huchukua muda mrefu hadi kuisha,na hii hutegemeana na uwezowa mtu wa kuzuia hasira hiyo.Hali hii huonekanani ya kawaida sana na ya kuzoeleka kwa kuwa husababishwa na hisia juu ya kitu fulani,na kawaida ya hisia hubadilika muda baada ya muda.
Hivyo hasira huwa na faida zaidi pale unapokuwa na uwezo wa kujizuia na kuizuia,lakini huwa na madhara zaidi pale unaposhindwa kujizuia na hata kuizuia kwani huweza kukusababishia madhara makubwa kiafya,kisaikolojia na hata kimahusiano.

Nini chanzo cha hasira
Katika maisha ya kila siku tunakutana na mambo mengi sana ambayo kwa namna moja au nyingine na kwa mitazamo tofauti tunayokuwa nayo,yanaweza kusababisha au kupelekea mtu kupatwa na hasira.
Haijalishi jambo lina uzito au udog kiasi gani,lakini jambo hilo linapokupa au kukuamshia hisia tofauti na ulivyotegemea hasira huweza kutokea mara moja.Hivyo hasira kwa kiasi kikubwa husababishwa na hisia juu ya mambo haya yafuatayo:
  • Kuumizwa kwa njia yoyote ile bila sababu yoyote ile,hiihutokea zaidi katika mahusiano hasa ya kimapenzi.
  • Kulazimishwa kufanya jambo au kitu usichokipenda
  • Kutokutendewa haki unayostahili bila kujalisha ni kweli ama si kweli.
  • Vitisho na mawazo ambayo hupendezwi nayo katika maisha yako.
  • Msongo wa mawazo pia ni chanzi kikubwa cha hasira,kwani mtua anapopata msong wa mawazo maana yake anakua na mkusanyiko wa mambo mengi sana kichwani ambayo yamekosa suluhisho la kuyapunguza. Hivyo anakuwa na uwezo wa kufanya chochote atakachoamua,hivyo hasira zake zipo karibu zaidi.
  • Kukataliwa katika jambo au mambo ambayo huamini kuwa na thamani katika maisha yake ya kila siku.
Pamoja na sababu nyingine nyingi ambazo hutofautiana kati ya mtu na mtu,na huwa na hisia otfauti,huweza pia kupelekea mtu kupatwa na hasira.
Kumbuka:Kitu kinachoweza kukufanya wewe kupatwa na hasira za mara kwa mara,kinaweza kumfanya mtu mwingine kuwa na furaha au kuwa katika hali ya kawaida.Hii yote hutokana na tafsiri juu ya jambo fulani ambapo tafsiri hiyo hupelekea kupatwa na hisia tofauti na uliyoitegemea katika jambo lile,na mwisho wake hupelekea kupatwa na hasira.Na hali huweza kupelekea ugumu katika kuielewa na kuizia hasira.

Nini Matokeo ya hasira
Hasira ni hali inayoweza kuzuilika,lakini pia kuna wakati hasira hushindwa kuzuilika na hatimaye mtu hukutana na changamoto zifuatazo katika mazingira tofauti:
  • Kushindwa kupata suluhisho la matatizo mbali mbali unayokutana  nayo katika maisha ya kila siku.
  • Kushindwa kufanya maamuzi sahihi pale unapokutana na hali inayohitaji maamuzi.
  • Kushindwa kujenga na kuimarisha mahusiano yaliyo imara na bora zaidi,haijalishi ni mahusiano ya aina gani.
  • Kupoteza uaminifu kwa watu wako wa karibu,na hii ni kutokana na jinsi unavyochukulia na kutafsiri mambo.
  • Huathiri zaidi utendaji na uwajibikaji katika majukumu ya kila siku kama vile biashara,masomo na hata shughuli za kiofisi.
  • Lakini pia mtu mwenye hasira za mara kwa mara huweza kuathiriwa kiafya na kujikuta amedhoofika sana.
Kuna utafiti uliofanywa na wasomi wa saikolojia huonyesha kuwa,mtu aliye na hasira za mara kwa mara huweza kupatwa na matatizo mengine kama vile;Ugonjwa wa moyo(Cardinal heart disease),matatizo ya kula(Eating disiorder).

Jinsi yaKuzuia Hasira
Unaweza kuzuia hasira yako pale unapoweza kuitambua mapema kabla haijawa na madhara kwako na kwa wengine pia.Hizi ni baadhi tu ya njia utakazoweza kutumia kuweza kuzuia hasira yako pindi utakapotambua kuwa imekaribia kuwa na madhara:
  • Tambua na kubali kuwa una tatizo,na hapo ndipo anza kupangajinsi ya kukabiliana hna hilo tatizo.
  • Tambua na uelewe kwa umakini na utulivu wa hali ya juu chanzo au vyanzo vya hasira yako kwa mtazamo chanya.
  • Shirikisha watu wako wa karibu na unaowaamini zaidi juu ya tatizo ulilo nalo,famili na rafiki zako wa karibu ndio watu wa muhimu zaidi.
  • Ingilia na zuia mzunguko wako wa hasira pale utakapoanza kuhisi hasira hasa kwa kutumia mbinu tofauti(Relaxation techniques) kama kuvuta hewa ndani kwa muda na kuitoa taratiiibu.
  • Chukulia tatizo linalikupa hasira kam ni la mwenzako na uhisi kama ni yeye,ungelichukuliaje(Empathy).Kumbuka kila mtu hukosea,na kupitia kukosea tunajifunza.
  • Weka na tengeneza furaha katika maisha yako,na uchukulie changamoto kwako kama ni ushindi.Hapo utakua umeshinda kila kitu.Jifunze kucheka na kufurahi kila siku.
  • Jifunze kuwa msikivu na muelewa kwa kila kitu,kwani kutofautiana katika mawasilia ni chanzo pia cha hasira.
  • Siku zote kuwa na kiasi kwa kila unachokifanya,heshimu unachokipenda na uheshimu pia uhitaji wa mwenzio.
  • Jifunze kuishi kwa muda na kufanya maisha yako kama yapo katika siku za mwisho.Kumbuka maishani mafupi sana,unapotumia muda mwingi kuwa na hasira unapunguza kwa kasi kubwa sana hizo siku zko chache zilizobaki.
  • Mwisho,SAMEHE NA SAHAU.
Kumbuka: Anza leo kupatana na kila umwonaye hukusababishia hasira,najua ni ngumu sana kwa mazingira ya kawaida.Lakini ukiamua kujishusha na kufikiria kuwa bado una mambo mengi ya kufanya na hayajakamilika,huwezi kuziruhusu hisia zako kuwaza vibaya na hatimaye kukupeleka usipopataka.Na hapo utakua umepiga hatua kubwa sana katika maisha yako.

Comments

Popular posts from this blog

JE,WAJUA KUWA UNA TATIZO LA KISAIKOLOJIA?

NINI CHANZO CHA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO?