ITAMBUE SONONA(DEPRESSION)
Sonona(Depression) ni mojawapo ya magonjwa ya akili ambayo madhara yake katika mustakabali wa maisha ya mtu binafsi pamoja na watu wanaomzunguka sio mazuri sana,madhara haya huweza kuleta hali ya sintofahamu kwa watu wanaomzunguka mtu aliye katika hali hiyo wakati mtu mwenyewe aliye katika hali ile hujiona kawaida kwa kuwa ndio hali inayomfanya ajisikie ahueni.
Sonona(Depression) ni hisia za huzuni na masononeko azipatazo mtu kutokana na matokeo ya mifumo mbalimbali ya maisha kama vile mahusiano,shule,kazi na mambo mengine yanayochukua nafasi ya muhimu katika maisha ya mtu binafsi. Hisia hizi ambazo mara nyingi huwa katika mfumo hasi,hutokana na matokeo yasiyotarajiwa na mtu katika jambo fulani ambalo anaweza kuwa alilipa nafasi kubwa sana katika maisha yake,lakini jambo hilo likatokea kuwa tofauti na kuingilia au kuvuruga kwa kiasi kikubwa mfumo wa kufikiria na kutenda wa mtu.
Zitambue dalili za mtu mwenye Sonona(Depression)
- Kujisikia huzuni na maumivu ndani ya nafsi(Depressed mood)
- Kukosa hamu ya kufanya au kujihusisha na jambo lolote lile hata kama ni jambo ambalo ulikua ukifanya unafurahia(Loss of interest)
- Kupungua au kukosa kabisa hamu ya kula chakula,hali hii hupelekea mtu kujikuta akipungua zaidi au kuongezeka uzito(Changes in appetite)
- Kupata shida ya usingizi,na hii huweza kuwa ama mtu kulala sana hasa nyakati za mchana au kukosa kabisa usingizi hasa nyakati za usiku(Trouble sleeping)
- Hali ya kukosa au kupungukiwa nguvu mwilini,na hatimaye kushindwa kufanya shughuli za msingi au hata utambuzi wa vitu na watu(Loss of enegry)
- Kupata shida katika kufikiria,kufanya maamuzi na hata kushindwa kabisa kuconcentrate kwenye jambo moja.(Difficulty in thinking,concentration and decision making)
- Kubwa na mbay zaidi ni kusumbuliwa au kukumbwa na mawazo ya kujidhuru(Suicidal thoughts)
Lakini dalili hizo pekee hazitoshi kumaliza kwamba mtu anasumbuliwa na sonona,bali dalili hizo tajwa hapo juu zinatakiwa kuonekana kwa mtu sio chini ya mda wa majuma matatu. Na tafiti mbalimbali za kisaikolojia zinaonyesha kwamba ,sonona hukadiliwa kuathiri watu 2 kati ya watu wazima 16 kwa kila mwaka. Na wahanga wakubwa zaidi wa Sonona(depression) ni wanawake tofauti na wanaume,ambapo tafiti zinaonyesha kwamba zaidi ya moja ya tatu ya wanawake hukumbwa na sonona kila mwaka.
Thank you for the message.
ReplyDelete