CHANZO CHA UKOROFI NA UTUNDU

Familia nyingi sana hasa wazazi mara nyingi hulalamika sana juu ya baadhi ya tabia za watoto wao ambazo huonekana ni chanzo cha migogoro ama katika familia ama katika jamii inayoizunguka familia hiyo. Tabia hizi huonekana kuwa si kero tu bali ni usumbufu wa hali ya juu sana,kwani huwafanya wazazi kupoteza muda kwa kiasi kikubwa katika kuhakikisha hali inakuwa shwari.

 
Kutokana na kutokuwepo kwa hali ya ukaribu zaidi kati ya wazazi na watoto,hali hii imekuwa ni ngumu sana kwani baadhi ya wazazi wamekosa na hawana njia sahihi ya kukabiliana na hali hii.
Lakini ukweli ni kwamba hali hii inayowakumba watoto wengi ni matokeo ya kisaikolojia,ambapo mtoto anapokuwa mdogo zaidi kutokana na hatua mbalimbali za ukuaji anazopitia,ama kuna hatua fulani hakuipita vizur ama hakuipitia kabisa. Na mwisho wake amejikuta akikosa changamoto za muhimi ambazo huweza kumfanya kujifunza baadhi ya vitu ambavyo ni muhimu sana.
Ukosekanaji ama upungufu wa ukaribu kati ya mtoto na mzazi huweza kumsababishia kwa kiasi kikubwa mtoto kuwa na hali ambayo huonekana kumkera mzazi katika wakati huu ambao ambao amejikuta akiwa karibu na mwanae huyo.Ukaribu kati ya mzazi na mtoto wakati wa ukuaji ni njia kubwa sana ya kisaikolojia ya kumfany mtoto wako kuwa kama unavyotaka na kubehave katika tabia sahihi.
Mtoto anapokaa mda mrefu sana akiwa mbali na wazaza hadi kufikia muda wa kujitambua,huweza kuwa mtu wa tofauti sana kutokana na kukosa attachment kutoka kwa wazazi,na hii humpelekea kuwa msumbufu na asiyetulia.Aliye na mabo mengi sana na mengine hata hayan umuhimu wowote.
Kwa hiyo tabia nyingi sana za ukorofi ambazo tunawaona nazo watoto wengi hutokana na sababu kubwa kama hizo nilizoelezea hapo juu. Na matokeo yake mtoto huyo huweza kupata ugonjwa unaoitwa ADHD(Attention Deficit Hyperactivity Disiorder)

Comments

Popular posts from this blog

NI NINI CHANZO CHA HASIRA

JE,WAJUA KUWA UNA TATIZO LA KISAIKOLOJIA?

NINI CHANZO CHA MIGOGORO KATIKA MAHUSIANO?